Bwana Peter W. Kifunguomali (Miaka 41 – Mtanzania)
Afisa Mtendaji Mkuu/ Katibu wa Bodi
Ndugu Kifunguomali ana Shahada ya Uzamili katika masuala ya Biashara ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Jamia Millia Islamia, New Delhi, mwaka 2014 na Shahada ya Sayansi ya Uchumi katika kubuni Miradi na kuisimamia kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe mwaka 2007. Aliwahi kufanya kazi katika Wizara ya Mali Asili na Utalii, Benki ya NBC na Mfuko wa LAPF. Kabla ya wadhifa wake wa sasa kwenye Kampuni, alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Mipango cha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Watumishi wa Umma (PSSSF) tangu Septemba, 2018. Alikuwa ni Mjumbe wa Bodi ya Kampuni toka Julai 2017 hadi June, 2019.
Bwana Joel Chikoma (Miaka 36 – Mtanzania)
Msimamizi wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu
Bwana Chikoma ana Shahada ya masuala ya Usimamizi wa Biashara na Uhasibu kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini. Anatambulika kama Certified Public Accountant (CPA (T) mwaka 2013 na Certisfied Risk Management Proffessional (CRMP). Ameitumikia Kampuni kwa miaka mitano tangu alipojiunga mwaka 2015 kama Mhasibu/ Afisa Uwekezaji. Aliwahi kufanya kazi TANROADS kama Mhasibu kwa miaka miwili na baadaye alijiunga na World Vision International kama Afisa wa Fedha na Utawala.
Bi. Rose Aloyce Osima (Miaka 40 – Mtanzania)
Msimamizi wa Kitengo cha Rasilimali Watu, Uongozi na Teknohama
Bi. Osima ana Shahada katika mambo ya TEHAMA (BSc. ICT) kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Pia ana Cheti katika masuala ya TEHAMA kutoka Kituo cha Compyuta cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na pia ana Stashahada ya Sayansi ya Kompyuta kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Bi. Osima alijiunga na Kampuni mwaka 2008 kama Mtaalam wa TEHAMA Katibu Muhstasi (IT-Assistant cum Secretary). Januari, 2011 alipandishwa cheo na kuwa Msaidizi wa Afisa Mtendaji Mkuu. Anaitumikia Kampuni kama Mtaalam wa TEHAMA.
Bi. Nancy C. Msisi (Miaka 37 – Mtanzania)
Msimamizi Msaidizi wa Ofisi (Rasilimali Watu na Uongozi)
Bi. Msisi alijiunga na Kampuni Aprili 2017 kutoka Benki ya EXIM kama Msimamizi Msaidizi wa Ofisi (OMA). Ana sifa zifuatazo: Stashahada katika Masoko kutoka Macmaine School of Business and Computing. Yeye alimaliza elimu ya sekondari mwaka 2007 kutoka Crane High School nchini Uganda.
Contact info
TCCIA Investment Company Limited [TICL] is a public limited liability company that was established by shareholders to expand financing sources to participate meaningfully in the ownership and control of the Tanzanian economy