Skip to main content

Bwana Fortunatus Magambo (Miaka 52 – Mtanzania)

Mwenyekiti
Ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi tangu mwaka 2018. Katika nafasi hiyo, mtazamo wake ni kubuni mikakati na sera za Kampuni, kuimarisha uongozi, na kukidhi matakwa ya wanahisa. Hivi sasa Bwana Magambo ni Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa Mfuko wa PSSSF na anauwakilisha Mfuko huo kwenye Bodi. Ni Mjumbe wa Bodi wa Nguru Hills Ranch Ltd, Benki ya Posta na  Ubungo Plaza Ltd. Ana uzoefu kwenye maeneo yafuatayo:-  Utawala, Uongozi, Mashirika, Usimamizi, Utafutaji na usimamizi wa miradi mikubwa na midogo, kuongea lugha mbalimbali, mashirika ya umma na mashirika binafsi. Amewahi kufanya kazi kama  Meneja wa Hazina wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii LAPF. Kupitia uzoefu wake, ameweza kuzisaidia Bodi nyingi kwenye Changamoto ya kifedha na kujiimarisha, kuendesha Biashara kubwa, kusaidia kukuza biashara mpya, na pia ana uwezo wa kuandaa Mpango Mkakakati kwa Maendeleo ya Shirika. Bwana Magambo alipata shahada yake ya kwanza kutoka Hanze University College – Groningen – Uholanzi, Shahada ya Uongozi wa Biashara katika masuala ya Fedha na Uhasibu, na ana shahada ya Uzamivu (Dutch Doctoral Programme – Doctorandus (Drs) - Associate Doctorate and MSc (Economics) – Kitivo cha Uchumi na Uongozi wa Biashara - kutoka Tilburg University - Uholanzi: Julai 2003.

Bwana Nathan Edward Mnyawami (Miaka 54 – Mtanzania)

Mjumbe
Bwana Mnyawami ana Shahada ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, 1993 na Shahada ya Uzamili ya Uchumi kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam, 2002. Bwana Mnyawami ana uzoefu wa miaka 20 katika kazi.  Kuanzia mwaka 1994 hadi 2002, alikuwa ameajiriwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kama Mtakwimu chini ya Mkurugenzi wa Masoko na Uwekezaji. Oktoba, 2002 hadi 2015 alijiunga na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Mashirika ya Umma (PPF) kama Mratibu/ Meneja wa Mipango na Utafiti. Alijiunga tena na TPDC mwaka 2015 kama Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji. Bwana Mnyawami ni mjumbe wa Kamati ya Uwekezaji na amesajiliwa na Chuo cha Wakurugenzi Tanzania (IoDT).

Bi. Magdalene Nelson Enock Mkocha (Miaka 67 – Mtanzania)

Mjumbe
Bi Mkocha ana shahada ya Sayansi katika Kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam, 1979, na shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine. 1988. Ana uzoefu wa kufanya kazi wa miaka 37. Kutoka Aprili 1979 hadi Juni 2002 aliajiriwa na Shirika la Kilimo na Chakula (NAFCO). Mwezi Julai 2002 alijiunga na Chama cha wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo Tanzania kama Afisa Mwandamizi wa Maendeleo wa TCCIA na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kilimo. Yeye ni mjumbe wa Kamati ya Ukaguzi na Athari za Kampuni. Bi Mkocha ni mjumbe wa Bodi/Kamati zifuatazo:- Baraza la Kazi, Uchumi na Ustawi la Wizara ya Kazi, Bodi ya Nyama Tanzania, Kamati ya Taifa ya Usafi, Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya VETA na mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Ushauri ya Bodi ya Sukari Tanzania. Pia amesajiliwa na Chuo cha Wakurugenzi Tanzania (IoDT).

Prof. Lucian Ambrose Msambichaka (Miaka 80 – Mtanzania)

Makamu Mwenyekiti
Prof. Msambichaka ana Shahada ya Kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Dar-s- Salaam, Shahada ya Uzamili na Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha   Leipzig Ujerumani. Prof. Msambichaka ni Mjumbe wa Bodi zifuatazo: Jumuiya ya Uchumi ya Kilimo Tanzania, Jumuiya ya Uchumi Tanzania na Utawala na Usimamizi wa Umma katika Jumuiya ya Afrika. Na pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji. Prof. Msambichaka amewahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi wa mashirika kadhaa ikiwepo Bodi ya Wakurugenzi ya Ngozi Morogoro, Taasisi ya Fedha ya Maendeleo ya Biashara, Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, Chuo Kikuu cha Biashara Moshi (MUCCOBS), Usajili wa Biashara na Utoaji wa Leseni  [BRELA], Mamlaka ya Maendeleo ya Bonde la Mto Rufiji (RUBADA), Chuo cha Ustawi wa Jamill na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Bwana Joseph Matanga Kahungwa (Miaka 58 – Mtanzania)

Mjumbe
Bwana Kahungwa ana shahada ya Biashara katika masuala ya Uhasibu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1987, na shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam, 2003. Pia yeye ni Makamu wa Rais (Kilimo) wa TCCIA tangu Mei 2013 mpaka sasa, mwanahisa na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Uwekezaji ya TCCIA na pia Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi. Bwana Kahungwa alikuwa Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza (Machi 2008 hadi Machi 2013). Hali kadhalika, alikuwa Makamu Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza (Machi 2001 hadi Machi 2008), Mjumbe wa Bodi ya CRDB Bank PLC kutoka mwaka 2001 hadi 2006, Mjumbe wa Kamati ya Fedha ya Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) kutoka 1977 hadi 2014. Awali, alikuwa na nyadhifa kama vile Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Pangea Minerals Ltd kutoka Julai 1999 hadi 2001, Mhasibu Mwandamizi - Pangea Minerals Ltd, Mhasibu Mwandamizi na Msimamizi wa Mikopo – Bodi ya Biashara ya Nje kutoka 1992 hadi 1994. Pia alikuwa Mhasibu wa Bodi hiyo kutoka 1991 hadi 1992. Amesajiliwa na na Chuo cha Wakurugenzi Tanzania (IoDT).

Bwana Paul Faraj Koyi (Miaka 60 – Mtanzania)

Mjumbe
Bwana Koyi ana shahada ya Sayansi katika masuala ya Elektroniki kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam. Kwa sasa yeye ni Rais wa TCCIA na Mwenyekiti Mtendaji wa BN`N Group of Companies. Pia alikuwa mjumbe wa Kamati ya Baraza la Biashara Tanzania, Mkoa wa Dar es Salaam, Mshauri anayejitgemea wa kampuni ndogo ndogo na za kati, Mkufunzi na Mshauri wa Vijana. Bwana Koyi amesajiliwa na Bodi ya Wahandisi (ERB) kama mwanataaluma. Pia amesajiliwa na EEU kama mshauri wa Tehama kwa miradi ya kusini mwa Afrika.

Bwana Ernest R. Khisombi (Miaka 55 – Mtanzania)

Mjumbe
Bwana Khisombi ana stashahada ya ADMA kutoka Chuo cha Uongozi wa Maendeleo cha Mzumbe (IDM), 1999 na shahada ya Uzamili katika masuala ya Uongozi wa Biashara kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, 2008. Sasa hivi yeye ni Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi wa Mfuko wa PSSSF na anawakilisha mfuko huo kwenye Bodi. Awali, alikuwa na nyadhifa kadhaa kwenye Mfuko NSSF kama Ofisa Mkuu wa Ugavi kutoka mwaka 2018 hadi 2019, Ofisa Mwandamizi wa Ugavi Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kutoka mwaka 2017 hadi 2018, Mkuu wa Kitengo cha Ugavi cha Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro na Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kutoka mwaka 2007 hadi 2017. Yeye ni mjumbe wa Kamati ya Ukaguzi ya TICL

Bwana Peter W. Kifunguomali (Miaka 41 – Mtanzania)

Afisa Mtendaji Mkuu/ Katibu wa Bodi
Ndugu Kifunguomali ana Shahada ya Uzamili katika masuala ya Biashara ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha  Jamia Millia Islamia, New Delhi, mwaka 2014 na Shahada ya Sayansi ya Uchumi katika kubuni Miradi na kuisimamia kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe mwaka 2007. Aliwahi kufanya kazi katika Wizara ya Mali Asili na Utalii, Benki ya NBC na Mfuko wa LAPF. Kabla ya wadhifa wake wa sasa kwenye Kampuni, alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Mipango cha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Watumishi wa Umma (PSSSF) tangu Septemba, 2018. Alikuwa ni Mjumbe wa Bodi ya Kampuni toka Julai 2017 hadi June, 2019.

Contact info

TCCIA Investment Company Limited [TICL] is a public limited liability company that was established by shareholders to expand financing sources to participate meaningfully in the ownership and control of the Tanzanian economy