Skip to main content

TCCIA Investment

  • WELCOME TO TCCIA INVESTMENT PLC
  • TOGETHER WE ARE STRONGER
  • WELCOME TO TCCIA INVESTMENT PLC
  • TCCIA INVESTMENT PLC
  • TOGETHER WE ARE STRONGER
Sisi TCCIA

Kampuni ya Uwekezaji ya TCCIA (TICL) ilisajiliwa  Novemba 9, 1999, chini ya Hati ya Usajili Na. 38280. Ni Kampuni ya Umma iliyoanzishwa na Chama cha Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima Tanzania (TCCIA) ikiwa ni juhudi za makusudi za kukuza vyanzo vyake vya mapato.

TCCIA ilitangaza uuzwaji wa Hisa za Awali – (IPO) ukihusisha-TCCIA Makao Makuu na  matawi yake ya mikoa na wilaya pamoja na wanachama  wake. Pia Mfuko wa Pensheni wa LAPF ulishirikishwa kama taasisi maalum ya uwekezaji.

Read More

“Kuwa kituo kikuu cha usimamizi wa uwekezaji Tanzania.

Kutengeneza ongezeko la thamani ya muda mrefu kwa wanahisa wa Kampuni kwa kutoa faida nzuri zaidi inayotokana na uwekezaji bora na salama.

Uwajibikaji, Kujitoa, Kufanya kazi kwa pamoja, Uaminifu na uvumbuzi.

Kwa Pamoja Tunaweza.

Wageni wetu

Ujumbe wa Ofisa Mtendaji Mkuu

Ninayo furaha na heshima isiyo kifani kuwakaribisha kwenye tovuti ya Kampuni ya Uwekezaji ya  TCCIA , ambayo inakupa upeo mpana wa kuelewa shughuli, kazi na huduma zetu. Tovuti hii inakupa picha kamili ya nini Kampuni yetu ya Kampuni ya Uwekezaji ya TCCIA inafanya – malengo yetu ya kuongeza thamani ya hisa na ukuaji wa Kampuni, azma ya kuunda kampuni tanzu na kubadili shughuli za Kampuni kutoka mifumo ya asili ya uwekezaji, kuboresha  thamani ya Kampuni kwa kuimarisha ukusanyaji wa rasilimali, kuongeza mapato ya uwekezaji, kuboresha michakato mbalimbali ya ndani kwa kuwatumia wafanyakazi wenye ari ya kujitolea na teknolojia ya kisasa ili kuboresha utendaji; kuboresha utoaji wa huduma za ndani kwa wateja; kuboresha utendaji kitaasisi; kujenga utamaduni wa utendaji kwa taasisi, na hatimaye kuboresha ustawi wa wafanyakazi, weledi na uzalishaji.

Kwa kweli, tuna ndoto na hamu ya kushuhudia fursa za kupendeza kwa siku za usoni kwa kutimiza malengo tuliyojikea kwa kampuni yetu.

Asanteni sana kwa kutembelea tovuti yetu. Ni matumaini yetu kwamba mtafurahia kuiangalia na kuona ubora wake. Pia, msikose kututembelea katika ofisi zetu za Dar es Salaam.

Mnakaribishwa kwa moyo mkunjufu

Together we are stronger

Contact info

TCCIA Investment Company Limited [TICL] is a public limited liability company that was established by shareholders to expand financing sources to participate meaningfully in the ownership and control of the Tanzanian economy