Wasifu
Kampuni ya Uwekezaji ya TCCIA (TICL) ilisajiliwa Novemba 9, 1999, chini ya Hati ya Usajili Na. 38280. Ni Kampuni ya Umma iliyoanzishwa na Chama cha Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima Tanzania (TCCIA) ikiwa ni juhudi za makusudi za kukuza vyanzo vyake vya mapato.
TCCIA ilitangaza uuzwaji wa Hisa za Awali – (IPO) ukihusisha-TCCIA Makao Makuu na matawi yake ya mikoa na wilaya pamoja na wanachama wake. Pia Mfuko wa Pensheni wa LAPF ulishirikishwa kama taasisi maalum ya uwekezaji.
Matokeo ya uuzwaji wa awali wa hisa za Kampuni (IPO) yaliiwezesha TCCIA pamoja na ofisi zake mikoani kulimiliki asilimia 1.2 ya hisa zote za Kampuni, -Hata hivyo, shukrani za pekee ziende kwa TCCIA kwa jitihada zake za kuanzisha Kampuni – ambayo iliweza kushiriki katika ununuzi wa Hisa za Benki ya NMB –
Kwa kutumia mtaji wake na hisa ndogo ilizonununua, TCCIA Investment PLC imeimarika na kuwa Kampuni ya uwekezaji ambayo inamilikiwa na Watanzania wenyewe.
Kwa nyongeza tu, Kampuni inasimamiwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) katika kundi la Uwekezaji wa Pamoja (Collective Investment Scheme). Mfumo huu unaiwezesha Kampuni Kuwekezeza katika vyanzo mbali mbali vya mapato.
Kampuni ilisajiliwa Novemba 1999 na kuanza shughuli zake za kibiashara Januari, 2005.
Kampuni iliamua kujikita katika uwekezaji wa hisa za kampuni zilizoorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Hii ina maana kwamba thamani ya kampuni inaweza kubainishwa wakati wowote kwa kuangalia maeneo mengine ya uwekezaji.
Hadi Desemba 31, 2019, jumla ya wanahisa wa Kampuni ilikuwa 3,432 ambapo Mfuko wa Pensheni wa LAPF ulikuwa ndiyo unaoongoza kwa kuwa na asilimia 38.5 ya hisa zote. Wanahisa waliobaki ni watu binafsi na mashirika machache yanayojishughulisha na biashara ndogo ndogo na za kati.
Kuanzishwa kwa kampuni na Shughuli zake
TCCIA Investment PLC (DSE: TICL), ni Kampuni ya Umma iliyoanzishwa na wanahisa ili kupanua wigo wa vyanzo vya mapato kwa ajili kushiriki kikamilifu katika kumiliki na kuendesha uchumi wa Tanzania. Kampuni ilianzisha uuzaji wa hisa zake kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam Machi 2018. Kampuni inadhibitiwa na kusimamiwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).
Kwa mujibu wa Katiba ya Kampuni (Memorandum and Articles of Association), au kwa kifupi MEMART, shughuli muhimu za TICL zinahusu uwekezaji kwenye mashirika ya kibiashara, viwanda, taasisi za fedha, mawasiliano kilimo, madini, ujenzi, mashamba/ viwanja na sekta ya huduma.
Majukumu ya Kampuni yameonyeshwa katika Katiba yake – MEMARTS – ambayo ni kukusanya na kuelekeza rasilimali fedha kutoka kwa wanahisa na kuzielekeza kwenye vitega uchumi muhimu. Vitega uchumi hivi vimegawanyika katika makundi mawili muhimu: vitega uchumi vya muda mfupi na muda mrefu