Bwana Kahungwa ana shahada ya Biashara katika masuala ya Uhasibu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1987, na shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam, 2003. Pia yeye ni Makamu wa Rais (Kilimo) wa TCCIA tangu Mei 2013 mpaka sasa, mwanahisa na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Uwekezaji ya TCCIA na pia Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi. Bwana Kahungwa alikuwa Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza (Machi 2008 hadi Machi 2013). Hali kadhalika, alikuwa Makamu Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza (Machi 2001 hadi Machi 2008), Mjumbe wa Bodi ya CRDB Bank PLC kutoka mwaka 2001 hadi 2006, Mjumbe wa Kamati ya Fedha ya Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) kutoka 1977 hadi 2014. Awali, alikuwa na nyadhifa kama vile Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Pangea Minerals Ltd kutoka Julai 1999 hadi 2001, Mhasibu Mwandamizi - Pangea Minerals Ltd, Mhasibu Mwandamizi na Msimamizi wa Mikopo – Bodi ya Biashara ya Nje kutoka 1992 hadi 1994. Pia alikuwa Mhasibu wa Bodi hiyo kutoka 1991 hadi 1992. Amesajiliwa na na Chuo cha Wakurugenzi Tanzania (IoDT).
Mjumbe
Contact Info
Education